DKT MWIGULU AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BELARUS



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Belarus, Mhe. Maxim Ryzhenkov, kwa mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.


Pande zote zilijadili fursa za ushirikiano katika sekta za kilimo, uvuvi, elimu, afya pamoja na viwanda vya dawa (pharmaceuticals), zikilenga kuongeza uwekezaji, kubadilishana utaalamu na teknolojia, pamoja na kuongeza thamani ya uzalishaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Ryzhenkov aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo(Mb.)


Mheshimiwa Ryzhenkov, yupo nchini kwa ziara ya kikazi hadi Aprili 30, 2026, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Belarus.









No comments