NAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO HAMISI MWINJUMA ASEMA SUALA LA KUHAMISHWA AFCON 2027 HALIPO


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa, suala la kuhamishwa kwa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027) kutoka Afrika Mashariki kwenda sehemu nyingine halipo.


Amesema hayo baada ya kumaliza kikao na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Samson Adamu kilichofanyika Aprili 23, 2026 Kampala Uganda, ambacho kiliwakutanisha nchi wenyeji wa mashindano hayo ambayo ni Tanzania, Kenya na Uganda.


No comments