UBORESHAJI SEKTA YA ELIMU AFYA MAJI NA MIUNDOMBINU WALENGA KUIMARISHA USTAWI WA JAMII



WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa juhudi ambazo zimefanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta za afya, elimu, maji na miundombinu zimelenga kuimarisha ustawi wa Watanzania.


Amesema hayo leo Mei 8, 2026 akiwa katika eneo la Magoweko, wilayani Gairo, mkoani Morogoro, ambapo aliwasisitiza wakazi hao watunze amani kwani ndiyo mtaji wa uhai wao. 


“Gairo kukiwa na amani watu wa kwanza kunufaika ni wanaGairo wenyewe. Kukiwa na uvunjifu wa amani, watu wa kwanza kuathirika ni wanaGairo wenyewe na amani ikipotea inahatarisha uhai wetu.”

 

“Kila ninakopita ninawakumbushia Watanzania kuwa mtaji wa kwanza wa kufanya shughuli yoyote ni uhai Mungu aliotupatia. Mtaji wa pili wa kufanya shughuli yoyote unayoiwaza ni amani katika eneo lako ulipo.”














No comments