MCHENGERWA AZINDUA MIRADI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO MUHIMBILI
Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, leo Septemba 30,
2026, amefika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini pamoja na miradi mbalimbali inayolenga
kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini.
Katika hafla hiyo, Waziri Mchengerwa anashiriki uzinduzi wa
Theatre mpya ya Mama na Mtoto pamoja na mtambo wa gesi ya oksijeni, miradi
inayolenga kuongeza uwezo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kutoa huduma
salama, za kisasa na zenye ufanisi kwa wananchi.
Kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi, Waziri Mchengerwa
ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika hospitali hiyo,
akipata maelezo kuhusu hatua za utekelezaji na namna miradi hiyo itakavyosaidia
kuboresha huduma kwa wagonjwa.
Theatre mpya ya Mama na Mtoto inatarajiwa kuongeza uwezo wa
hospitali katika kutoa huduma za kibingwa kwa wanawake na watoto, hususan
katika huduma zinazohitaji uangalizi maalumu na mazingira salama ya upasuaji.
Aidha, uwepo wa mtambo wa gesi ya oksijeni unalenga
kuimarisha upatikanaji wa oksijeni kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji huduma
hiyo wakati wa matibabu, hivyo kuongeza uwezo wa hospitali kukabiliana na
mahitaji ya huduma za afya.
Uzinduzi wa miradi hiyo pamoja na Bodi ya Wadhamini
unaakisi hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kuimarisha miundombinu na uwezo
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambayo ni miongoni mwa vituo muhimu vya huduma
za kibingwa nchini.
Hatua hiyo pia inalenga kuwezesha wananchi wanaohitaji
huduma za kibingwa, hususan Mama na Mtoto, kupata huduma katika mazingira yenye
miundombinu na vifaa vinavyokidhi mahitaji ya kisasa ya utoaji wa huduma za
afya.
Waziri Mchengerwa ameendelea na ziara hiyo kwa kushuhudia
uzinduzi rasmi wa miradi hiyo pamoja na shughuli nyingine zinazohusiana na kuimarisha
huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.







.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


Post a Comment