RAIS ZANZABAR DKT MWINYI ATUMA SALAMU ZA POLE KWA RAIS DKT SAMIA KUFUATIA KIFO CHA MUME WAKE
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, ametuma salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Hafidh Ameir Hassan.
Hafidh amefariki dunia leo, Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za msiba huo na kuungana na Rais Dkt. Samia, familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi.
Amesema msiba huo ni mkubwa kwa familia na wote waliokuwa karibu na Marehemu, huku akimuomba Mwenyezi Mungu awape Rais Samia na familia yake subira, nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.
Rais Dkt. Mwinyi pia amemuomba Mwenyezi Mungu amsamehe na amrehemu Marehemu Hafidh Ameir Hassan na amjaalie makazi mema peponi.
Hafidh Ameir Hassan anatarajiwa kuzikwa leo Kizimkazi, Zanzibar, katika mazishi yatakayohudhuriwa na familia, ndugu, jamaa, viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na wananchi.


Post a Comment