TAIFA STARS YAELEKEA MOROCCO KWA MECHI YA KUFUZU AFCON 2027



Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo Septemba 26, 2026, imeondoka nchini kuelekea Casablanca, Morocco, kwa ajili ya mchezo wa pili wa Kundi L wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Taifa Stars inaelekea Morocco baada ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa kampeni hiyo dhidi ya Guinea-Bissau, uliochezwa jana Septemba 25 katika Uwanja wa New AmaanComplex, Zanzibar. Tanzania ilipoteza mchezo huo kwa mabao 2-0. 

Mchezo unaofuata wa Taifa Stars utakuwa dhidi ya Madagascar, Septemba 29, 2026, jijini Casablanca, ambapo Madagascar imechagua Morocco kuwa mwenyeji wa mchezo huo.

Taifa Stars, chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi, inatarajiwa kutumia safari hiyo kujiandaa kwa mchezo huo muhimu wa Kundi L, baada ya kuanza kampeni kwa matokeo yasiyoridhisha dhidi ya Guinea-Bissau.

Tanzania iko Kundi L pamoja na Guinea-Bissau, Madagascar na Nigeria. Hata hivyo, Tanzania tayari ina nafasi ya kushiriki AFCON 2027 kutokana na kuwa mmoja wa wenyeji wa mashindano hayo pamoja na Kenya na Uganda. Kwa mujibu wa CAF, katika makundi yenye wenyeji hao, timu moja ya ziada ndiyo itakayofuzu pamoja na mwenyeji.

No comments