Serikali itaendelea kuhimiza matumizi ya teknolojia mahali pa kazi

 


NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Denis Londo (Mb), amesema Serikali itaendelea kuhimiza matumizi ya teknolojia mahali pa kazi ili kuboresha utekelezaji na utendaji wa kazi.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo wakayi wa ufunguzi wa mkutqno wq baraza la wafanyakazi wa Brela uliofanyika mkoani Morogoro na kuipongeza wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa hatua ilizochukua kuboresha Mfumo wa Huduma kwa Njia ya Mtandao (BRELA Online Services – BOS).


Amesema matunizi hayo ya teknolojia yatasaidia kuboresha utendaji kazi sambamba na luongeza ufanisi wa utoaji huduma.



Aidha, ameitaka BRELA kuendelea kufanya mapitio na maboresho ya sheria na kanuni mbalimbali kwa kushirikiana na wadau, kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na kurahisisha utoaji wa huduma nchini na kuongeza kuwa mchakato huo unapaswa kuwashirikisha wadau kikamilifu ili kupunguza urasimu, kuondoa masharti yanayokwamisha shughuli za biashara na kuimarisha uzingatiaji wa sheria.


Kwa upande wake Bw. Elias Kalist, akimwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara BRELA, amesema Bodi inatambua na kuthamini jitihada zinazofanywa na taasisi katika kuimarisha matumizi ya teknolojia na kuboresha utoaji wa huduma.

No comments