Dkt. YONAZI AHIMIZA MIPANGO ENDELEVU YA UENDELEZAJI MJI WA SERIKALI.

 


KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, amehimiza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuweka mikakati endelevu itakayohakikisha uendelezaji na usimamizi bora wa Mji wa Serikali Mtumba, kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na ya baadaye.


Dkt. Yonazi ametoa rai hiyo Novemba 24, 2026, jijini Dodoma, wakati wa kikao cha kupitisha mapendekezo kuhusu kuimarisha usimamizi wa ujenzi na uendeshaji wa Mji wa Serikali Mtumba.


Amesema ni muhimu kuwepo kwa mipango madhubuti na endelevu itakayowezesha Mji wa Serikali kuendelea kuimarika na kukidhi mahitaji ya Serikali kadri yanavyoongezeka, bila kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.


Aidha, ameupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi pamoja na kutumia mifumo ya kisasa katika kusimamia uendelezaji wa Mji wa Serikali.








No comments